Mshambuliaji James Rodriguez ajiunga na Everton kutoka Real Madrid
Klabu ya Everton imekamilisha uhamisho wa James Rodriguez kutoka Real Madrid kwa ada ya £20m. Mshambuliaji huyo raia wa Colombia, ambaye msimu uliopita aliichezea Madrid michezo 14 amepewa kandarasi ya miaka miwili. Alisajiliwa Real Madrid akitokea Monaco, mwaka 2014.
