Beyonce azindua rasmi video ya wimbo wa 'Brown Skin Girl'
Beyoncé amezindua video ya wimbo wake wa Brown Skin Girl ambayo ni moja ya nyimbo zilizo kutoka kwa albamu ya: The Lion King: The Gift. Siku ya Jumatatu, nyota hiyo iliweka video hiyo kwenye mtandao wa YouTubeambayo hapo awali ilikuwa inapatikana tu Disney kama sehemu ya filamu ya hivi karibuni ya, Black Is King.