Taylor Swift achanga kumsaidia mwanafunzi wa hisabati kutoka London

Mwimbaji Taylor Swift ametoa $ 23,000 kwa mwanafunzi kutoka London ambaye anajitahidi kupata pesa kuchukua kozi ya hisabati katika Chuo Kikuu cha Warwick. Nyota huyu wa kibao hiki cha You Need To Come Down aliandika ujumbe kwenye ukurasa wa kuchangisha pesa wa Vitoria kudhibitisha mchango wake.