Stephen Wamukota mbunifu wa miaka 9 aangaziwa

Maelezo ya sauti, wabunifu mashuhuri waangaziwa Afrika.

Huku idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona barani afrika ikifikia milioni, watu mbali mbali wanaendelea kubuni vifaa vya kupambana na changamoto za janga hili. BBC imeangazia wabunifu kumi mashuhuri ikiwemo Stephen Wamukota kijana wa miaka 9 aliyebuni kifaa cha kuosha mkono alichotengeneza kwa mbao. Ni ubunifu upi wakati huu wa janga la corona uliokufurahisha?