Mwanamziki Drake amevunja rekodi iliyowekwa na Madonna

Drake amevunja rekodi ya nyimbo nyingi Zaidi kuwahi kuwa katika kumi bora kwenye chati ya Marekani ya Billboard akivunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na mwanamziki wa pop Madonna. Ufanisi huu unakuja miaka 11 baada ya kibao chake cha kwanza kuwa kwenye chati hiyo kitengo cha kumi bora cha Best I Ever Had.