Wazee wapata umaarufu kwenye mtandao wa Instagram
Kwa miaka 70 bi Hsu Hsiu-e na mume wake Chang Wan-ji,wamekuwa wakioshea watu nguo mjini Taichung, katikati mwa Taiwan. Mjukuu wao aliwashawishi kuvaa nguo ambazo watu wanaziacha au hawazitaki tena na kisha akawapiga picha na kuziweka kwenye mtandao wa Instagram. Kwa mshangao wao wamepata umaarufu si haba.
