Kim Kardashian West azungumzia afya ya akili ya mumewe Kanye West

Maelezo ya sauti, Kim Kardashian West azungumzia afya ya akili ya mumewe Kanye West

Baada ya mwanamziki Kanye West kuandika msururu wa ujumbe kwenye ukurasa wa Twitter, uliozua wasiwasi kuhusu afya yake , sasa mkewe Kim Kardashian West ameomba watu wawe na huruma wakati huu Kanye anapopitia changamoto ya afya ya akili. Kanye ni mmoja wa wanamziki tajika akivuma kwa vibao kadhaa ikiwemo Stronger.