Corona: Raia wa Uingereza wageukia kunywa chai na biskuti.
Utafiti unaonyesha kuwa raia wengi nchini Uingereza wamegeukia kunywa chai, kahawa na kula biskuti kwa wingi pamoja na kusoma vitabu wakati huu wa janga la corona. Shirika la utafiti wa masoko linasema wainngerea wametumia pauni milioni £24m kwa chai na kahawa na pauni milioni £19m kwa biskuti kwa mda wa miezi mitatu. Je, ni chakula kipi kinachokupa utulivu wakati huu wa janga la corona? Sema nasi kwenye ukurasa wa Facebook, BBCNewsSwahili.
