Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wezi wamevunja duka la kuuza pombe na kuiba Whiskey
Siku mbili tu baada ya serikali ya Afrika Kusini kurudisha marufuku ya kuuza na kununua pombe ili kupambana na maambukizi ya virusi vya corona, wezi wamevunja katika duka moja la kuuza pombe huko Cape Town na kuiba kabati lote lililokuwa na pombe aina ya Whiskey. Maajabu ni kwamba mwenye duka anasema kuwa pombe aina ya Brandy na ile ya Wine haikuguswa hata! Nini maoni yako kuhusu kisa hiki? Sema nasi kwenye ukurasa wetu wa Facebook, BBCSwahili.