Timu ya Arsenal yaendelea kushindwa kwenye Ligi ya England
Masaibu ya Arsenal yameendelea-wiki baada ya wiki kichapo. Hapo jana walicharazwa na Tottenham HotSpurs kwa mabao 2-1 katika dabi ya London Kaskasini. Arsenal sasa imesalia katika nafasi ya tisa kwenye msimamamo wa ligi wakiwa na alama hamsini huku wakisalia na michezo mitatu kabla ya ligi ya England kumalizika.
