Corona: Nyota wa pop Lady Gaga asihi mashabiki wake wavae barakoa
Nyota wa kibao cha "Rain on Me" Lady Gaga aliweka picha kwenye mtandao wa Instagram akiwa amevaa barakoa ya nembo inayoangazia albamu yake mpya ya Chromatica wakati huu na kusihi mashabiki wake wabakishe uhalisia wao lakini pia wavae barakoa ili kujilinda wao, jamii yao na ulimwengu kwa jumla.
