The Rock ndiye 'mtu tajiri zaidi' kwenye mtandao wa Instagram.
Muigizaji maarufu Dwayne "The Rock" Johnson amekuwa nyota ambaye anaweza kulipisha malipo ya bei ya juu Zaidi kwa matangazo ya biashara kwenye ukurasa wa Instagram. The Rock anaweza kulipisha dola milioni moja kwa tangazo moja tu. Je unaweza kutumia ukurasa wako kulipisha matangazo ya biashara? Tupe maoni yako kwenye ukurasa wetu wa Facebook, BBCSwahili.
