Brazil: Kwa nini makaburi haya yamechimbwa ufuoni?

Maelezo ya sauti, wanaharakati waonesha hasira zao kwa serikali ya Brazil

Wanaharakati wa Brazil wanaoikosoa serikali yao namna inavyoshughulikia janga la corona kwa kuchimba makaburi mia moja katika ufuo wa bahari wa Copa-cabana mjini Rio die Janeiro. Tembelea tovuti ya BBC utazame makaburi hayo yaliowekwa msalaba mweusi, na mabango kuwaomboleza zaidi ya watu elfu 40 waliofariki na maradhi ya Covid-19.