Raheem Sterling: Soka ulaya inahitaji meneja wa asili ya KiAfrika

Maelezo ya sauti, Raheem Sterling: Soka ulaya inahitaji kuwa na meneja wa asili ya KiAfrika

Maendeleo katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi yatakuja tu kwenye sekta ya mpira wa miguu pale watu weusi zaidi watapewa nafasi zakuwa mameneja, mchezaji wa England na Manchester City Raheem Sterling anasema. Maelfu ya watu wameshiriki kwenye maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Uingereza, kufuatia kifo cha George George Floyd..