Mashabiki wa bendi ya BTS wachangisha dola milioni moja.
Mashabiki wa bendi ya mziki ya BTS wanaojiita 'Army' wamechangisha dola milioni moja kwa harakati ya 'Black Lives Matter', baada ya habari kuwa wanabendi hao pia walichangisha dola milioni moja kwa kampeni hiyo. Kampeni Black Lives Matter inayoendelea nchini Marekani inatetea dhuluma na ubaguzi wa rangi unaofanyiwa watu weusi nchini humo.
