Mchezaji aonesha tisheti ya "haki kwa George Floyd"

Maelezo ya sauti, Jadon Sancho aonesha tisheti ilionadikwa haki kwa George Floyd

Mchezaji wa timu ya Borrusia Dortmund Jadon Sancho pamoja na wachezaji wengine wa ligi ya Bundesliga hawatachukuliwa hatua baada ya kutoa matamshi ya kupinga ubaguzi wa rangi kwenye mechi zilizochezwa wikendi.Sancho alivua jezi lake na kuonesha tisheti iliyokuwa imeandikwa “Haki kwa George Floyd” baada ya kutinga goli dhidi ya timu ya Paderborn.Floyd ni mmarekani mweusi alieuwawa mikononi mwa polisi wiki iliopita.