Mwanamuziki kutoka Denmark atumbuiza mashabiki wake.

Usikose kuagalia tovuti ya BBC uone jinsi mwanamuziki kutoka Denmark Mads Langer alivyofanya tamasha la muziki kwenye eneo la kuegesha magari katika uwanja wa ndege wa Copenhagen.

Mads alitumbuiza mashabiki wake waliokuwa ndani ya magari yao huku wakifuata masharti yote yaliowekwa kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.