Wanamziki Liam na Alesso wamezindua video ya 'Midnight'
Licha ya changamoto zilizoshamiri za janga la virusi vya corona ikiwemo marufuku ya kutoka nje, hazijawazuia wanamuziki Liam Payne na Alesso kutoka Uingereza na Marekani kurekodi video ya wimbo wao mpya wa Midnight. wamejitahidi na kufanya video zao wakiwa nyumbani kwao kisha zikachanganywa pamoja na mtayarishaji wa video za mziki Conor Butler.
