Virusi vya corona: Wakazi 'wanavyotishwa' kudhibiti corona Indonesia
Kijiji kimoja nchini Indonesia kinahimiza raia wake kusalia majumbani na kukaa umbali wa mita moja, kwa kuwatumia watu wanaovaa mavazi ya kutisha ya kishetani ili kuwashtua masaa ya usiku. Hatua hio imechukuliwa baada ya baadhi ya watu kutozingatia maagizo yaliotolewa ili kudhibiti virusi vya Corona. Je, unadhani mbinu hii inaweza kufanya kazi katika eneo lako?
