Virusi vya corona: Tamasha la pasaka lanoga mtandaoni
Nyota maarufu wa nyimbo za Classic Andrea Bocelli amefanya tamasha wakati huu wa pasaka huko Milan na kuimba peke yake katika kanisa maarufu la mji huo. Tamasha hio kwa jina Music for Hope, ilipeperushwa moja kwa moja kwenye mtandao wa Youtube na kupata milioni ya jumbe za shukran kutoka kwa watazamaji ambao wanaendelea kutekeleza marufuku ya kutotoka nje wakati huu wa pasaka.
