Muigizaji atishiwa maisha yake kwa sababu ya kudansi
Nermine Sfar muigizaji kutoka nchini Tunisia amesema amepokea vitisho dhidi ya maisha yake kutoka kwa kundi la jihadi baada ya kuanza kupeperusha video za moja kwa moja akicheza kwenye mtandao wa Facebook kwa madhumuni ya kuwatumbuiza watu waliofungiwa manyumbani kufwatia janga la Corona.
