Je, filamu ya 'Cats' ndiyo mbaya zaidi kuwahi kutokea?

Filamu ya Cats imepata tuzo nyingi zaidi za filamu mbaya zaidi za mwaka huu maarufu Golden Raspberry Awards. Filamu hiyo ya aina ya muziki ilipewa tuzo sita za Razzies, ikiwemo picha mbaya zaidi na mwingoza filamu mbaya zaidi akiwa ni Tom Hooper.