Ilikuwaje binti huyu kutoka Nigeria akaolewa na wanaume wawili?
Sakata ya mapenzi inaendelea katika jimbola Kaskazini Nigeria la Kano, ambapo wanaume wawili walioa mwanamke mmoja katika matukio mawili tofauti. Hauwa Ali Mariri mwenye umri wa miaka 32, ndiye mwanadada ambaye kwa sasa huenda akaadhibiwa iwapo atapatikana na hatia ya kuwapotosha wanaume hao wawili. Bello Ibrahim, mume wa kwanza, alirudi nyumbani na kumpata mwanamume mwingine amelala kitandani mwake. Nini maoni yako kuhusu tukio hili? Sema nasi kwenye ukurasa wa Facebook, BBCSwahili.