Uhaba wa nyanya Afrika Mashariki unasababishwa na nini?
Wakazi wa Afrika mashariki wamekuwa wakizungumzia kuadimika kwa nyanya siku za hivi karibuni. Katika baadhi ya masoko,nyanya inauzwa bei ya juu kuliko hata tufaha, tunda ambalo kwa kawaida huwa ndilo ghali mno maeneo mengi Afrika. Uhaba huu wa nyanya unadaiwa kusababishwa na mvua kubwa ambayo ilinyesha maeneo mengi mwishoni mwa mwaka jana.