Wanamziki Shakira, J-Lo wang'aa wakati wa Superbowl

Maelezo ya sauti, Wanamziki wa asili ya Latino Shakira na J-Lo wang'aa wakati wa Superbowl

Katika hafla kubwa kwenye kalenda ya michezo nchini Marekani maarufu kama, Super Bowl wanamziki Jenifer Lopez na Shakira wametumbuiza wakati wa mapumziko huku wakiimba nyimbo 20 kwa dakika 12 tu. Wawili hao wamemalizia kwa kuimba wimbo wa Shakira wa wakawaka ambao ulikuwa wimbo ramsi wa soka mwaka wa 2010.