Bendi ya muziki ya Sautisol yatamba kimataifa
Kundi la Sauti sol kutoka Kenya limetangaza kupitia mtandao wa Instagram kuwa limesaini mkataba na kampuni ya kurekodi muziki ya Universal na kwamba albamu yao mpya ya Midnightrain, inayotarajiwa kwa hamu na mashabiki wao itazinduliwa kupitia nembo hiyo ya Universal Music Group.
Sautisol wamejipatia umaarufu mkubwa kupitia vibao vyao kadhaa ikiwemo wimbo wa 'Short and sweet'.
