Je ni kwa nini viatu hivi vya kampuni ya Nike vinakashifiwa?
Shirikisho la mchezo wa riadha duniani linatarajiwa kuimarisha kanuni zake kuhusu viatu vya hali ya juu, kufuatia malalamishi kuhusu viatu vipya vya kampuni ya Nike vinavyojulikana kama Vaporfly. Eliud Kipchoge alivaa toleo la mwaka huu alipokuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia mbio za marathon kwa mda wa chini ya masaa mawili.
Lakini je, ni kweli kwamba viatu hivi vinaweza kumwezesha mwanariadha kushinda au kushindwa?