Eminem awajibu waliokosoa wimbo wake

Msanii wa Marekani wa muziki wa Rap Eminem amejibu wakosoaji wake wa hivi karibuni dhidi ya wimbo wake wa Unaaccomodating ambao umegusia shambulio la bomu la Manchester.Rapa huyo alilaumiwa kuimba kuhusu shambulio la bomu la Manchester lililosababisha vifo vya watu 22 kwenye tamasha la Ariana. Eminem amesema Albamu hiyo ilikuwa na lengo la "kutikisa dhamiri'', ambayo inaweza kusababisha hatua nzuri.