Barcelona yashinda Manchester United kwa mapato
Klabu ya Barcelona ndiyo iliyopata mapato mengi zaidi kuliko klabu yoyote ile barani ulaya kwa mara ya kwanza msimu huu. Klabu hiyo ya Uhispania imepata mapato ya pauni milioni 741.1. Real Madrid imeorodheshwa ya pili huku Manchester United ikiwa ya tatu.
