Sheria ya kiapo cha siri yaondolewa ili kuleta uwazi

Maelezo ya sauti, Papa Francis ameondoa kiapo cha siri kwa visa vya unyanyasaji wa kingono

Papa Francis ameondoa sharia ya zamani inayowapa usiri wanaotubu makosa ya unyanyasaji wa kingono katika jitihada ya kujaribu kuongeza uwazi katika kesi aina hiyo. Hapo awali kanisa liliona umuhimu wa kuweka swala hilo siri katika kile ilichosema ni juhudi za kulinda waathirika.