Nzige waliovamia wafukuzwa kwa kufyatuliwa risasi

Maelezo ya sauti, Nzige waliovamia maeneo ya Somaliland wafukuzwa kwa kufyatuliwa risasi

Watu katika jamhuri iliyojitangazia uhuru ya Somaliland wamefyatulia risasi kundi la nzige kujaribu kuwafukuza. Maeneo mengine yaliyoathiriwa na nzige, kama vile Ethiopia , watu wamekuwa wakipiga sufuria na vifaa vingine vya kupika kujaribu kuwatishia nzige hao. Je, ni njia ipi mwafaka ya kufukuza nzige? Tueleze kwenye ukurasa wa Facebook, wa BBCSwahili.