Africa Eye: Ushahidi wa uwezekano wa uhalifu wa kivita Sudan wazuka
Africa Eye: Ushahidi wa uwezekano wa uhalifu wa kivita Sudan wazuka

Uchunguzi uliofanywa na Idhaa ya BBC Arabic umebaini Ushahidi wa uhalifu wa kivita kutoka pande zote mbili katika mzozo wa Sudan , huku mfumo wa afya ukiporomoka.
Ni maeneo machache tu ya hospitali 88 za mji mkuu wa Khartoum ambayo yamesalia wazi baada ya wiki tano za mapigano kulingana na Muungano wa madaktari nchini Sudan.
Kwa kutumia data ya satelaiti, zana za kuchora ramani, maudhui yaliyotolewa na mtumiaji kwa kuzungumza na madaktari kadhaa, uchunguzi wa BBC Arabic umefichua ushahidi wa kutosha wa uwezekano wa uhalifu wa kivita kwenye vituo vya matibabu na wanajeshi wa pande zote mbili.



