Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Gabriel Geay: Niliona kumuacha Kipchoge inawezekana
Mwanariadha wa Tanzania Gabriel Geay jana Jumatatu alishinda kwa kumaliza wa pili katika mbio kongwe zaidi Duniani za 127 za Boston nchini Marekani kwa kumaliza mbio za Kilomita 42 kwa 2:06:04.
Hata hivyo Geay aliwashangaza wengi baada ya kumpiku mkongwe na ambaye amekua akishikilia rekodi mbalimbali za Dunia katika riadha Eliud Kipchoge kutoka Kenya tukio ambalo ni nadra kwa mwanariadha wa Tanzania.
Mwanariadha mwingine wa Kenya Evans Chebet alimshinda Benson Kipruto na kutetea vyema taji lake la Boston Marathon nchini Marekani.
Chebet alimshinda Gabriel Geay wa Tanzania hadi nafasi ya pili kwa saa 2:06:04 huku Kipruto akimaliza wa tatu kwa saa 2:06:06.
Lakini mwanariadha kutoka Tanzania Gabriel Geay ambaye anashikilia rekodi ya mbio kwa taifa la Tanzania na kushika nafasi ya pili huko Boston Jana Jumatatu anazungumziaje ushindi huo? Amezungumza na Scolar Kisanga