Kijana Mkenya aliyekaidi ulemavu kucheza soka ya kulipwa Uturuki
Kijana Mkenya aliyekaidi ulemavu kucheza soka ya kulipwa Uturuki

Chanzo cha picha, Munga
Wanamichezo wengi maarufu duniani wameshinda vikwazo vingi ikiwa ni pamoja na magonjwa na hata upasuaji kupata umaarufu.
Hata hivyo, kwa Mkenya Mohammed Munga, hali yake ya ulemavu imempa nguvu na ari ya kuwa mmoja wa wanasoka maarufu zaidi.
Munga anayeichezea timu ya taifa ya Kenya ya wachezaji wanaotumia magongo pia anacheza soka la kulipwa nchini Uturuki katika club ya Depsas huko Uturuki.
Mwandishi wa BBC Seif Abdalla Dzungu amezungumza na mchezaji huyo pamoja na familia yake na kutuandalia taarifa hii.
Video: Frank Mavura



