Je, ongezeko kubwa la bei ya mafuta nchini Tanzania lina maana gani?

Je, ongezeko kubwa la bei ya mafuta nchini Tanzania lina maana gani?

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini Tanzania, EWURA, imetangaza bei mpya za mafuta ambazo zimeanza kutumika Agosti pili.

Bei hizo zinaonesha mafuta ya petroli yamepanda bei kwa shilingi 443 na dizeli ikipanda kwa shilingi 391 kwa kila lita moja kwa mafuta yanayouzwa katika jiji kuu la kibiashara la Dar es Salaam.

Hali hii inaleta wasiwasi wa kupanda bei kwa bidhaa na huduma mbalimbali hususani zinazotegemea nishati ya mafuta kama vile chakula na usafirishaji.

Mchambuzi wa masuala ya kiuchumi kutoka chuo cha ushirika Moshi Tanzania, Beatrice Kimaro amezungumza na Regina Mziwanda kuhusu maana ya ongezeko hili ambalo ni kubwa zaidi katika miezi ya hivi karibuni.