Sindano za kuondoa mikunjo ya uso: Tiba ya kisasa ya kukabiliana na kipandauso

Chanzo cha picha, Getty Image
Zaidi ya watu bilioni moja duniani wanakabiliwa na maumivu yasiyoelezeka kutokana na athari za kipandauso au 'Migraines'.
Lakini utafiti unaongoza kwa matibabu mapya dhidi ya hali hii inayoumiza wengi.
Kila siku asubuhi baada ya kujiandaa, kupigwa mswaki na kujipaka mafuta, Megan Daniels hujiangalia kwenye kioo akisugua shingo yake na kifaa kidogo kama kiredio cha mkononi cha kupokea taarifa. Anakizungusha kutoka shingoni hadi mfupo wa taya akikiweka hadi aanze kuhisi kuwashwa ma eneo la mwisho la mdomo wake uanze kushuka kuelekea.
"Inatuliza, inahisi kana kwamba unatuma mtikisiko kwenye ubongo," anaelezea Daniels mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Liverpool nchini Uingereza.
Kila siku yeye hukanda shingo yake na kifaa hicho akiamka, wakati wa chakula cha mchana na kabla ya kulala.
Anatumia kifaa hicho kupunguza maumivu ya kipanduso au 'migraines'.
Kipandauso ni hali ya mfumo wa neva na huwaathiri zaidi ya watu billioni moja kote duniani.
Kwa waathiriwa wengi, ugonjwa huu hujitokeza kama kichwa kuuma na dalili nyingine nyingi kama kizunguzungu na kutoona mwanga vizuri.
Daniels hutumia kifaa hicho cha kupunguza makali ya kipandauso, kinachotumia umeme kusisimua seli za neva ambazo zinatoka shingoni kupitia usoni hadi kichwani.
Licha ya ugonjwa huu kuwaathiri wengi, sababu zinazochangia kipandauso hazijulikani na imebakia fumbo kwa wanasayansi wengi.
Ila wanasayansi wakiendelea kujaribu kulifumbua fumbo hili, wamekuwa wakivumbua njia mpya ya kuutibu ugonjwa huu.
Mara nyingi wale ambao huugua ugonjwa huu, huumwa kichwa kwa upande mmoja, wengine huhisi kichefuchefu na kutapika, wengine huumizwa na mwangaza mwingi, kelele na harufu.
Kwa 25% ya watu wanaougua ugonjwa huu hupata matatizo ya kuona.
Robo tatu ya wanaoathirika na ugonjwa huu ni wanawake. Ingawa waathiriwa wengi huwa watu wazima, watoto pia wanaweza kuathirika huku wengine wakipata maumivu makali ya tumbo.
Mbona ni vigumu sana kutibu kipandauso?

Chanzo cha picha, Getty Images/ BBC
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wanaougua ugonjwa huu chanzo kinakuwa ni mambo tofauti tofauti na kutibu magonjwa ya neva pia ni changamoto. Ingawa kuna wale ambao hupata suluhisho haraka, kuna wale ambao hujaribu mbinu tofauti za matibabu bila kufanikiwa.
'Mimi kama mgonjwa wa kipandauso, naweza kutuliza maumivu kwa kununua dawa za kupunguza maumivu ya kichwa kama paracetamol na ibuprofen,' anasema Daniels
Wanasayansi pia wamekuja na dawa ambazo zinakabiliana na changamoto hii kwa kulenga mishipa ya damu, kemikali za seratonini ambazo zinatuliza faiba za neva.
Ingawa tafiti zinaonyesha kuwa theluji tatu ya wagonjwa hupata
nafuu baada ya saa tatu baada ya kumeza dawa hizi kuna wengi ambao dawa hizi hazifanyikazi katika miili yao.
Pia kuna hatari ya kumeza dawa za kupunguza maumivu kila mara, kwani mara nyingi huongeza kichwa kuuma, kutokana na 'kutumia dawa za kupunguza maumivu ya kichwa kupita kiasi.'
Ila sio kutuliza maumivu tu, wagonjwa wengi hutaka tiba ya kuzuia maumivu hayo kutokea kwa sababu yaweza kuanza taratibu hadi kuwa jambo linalotokea kila siku.
Katika miongo kadhaa, madaktari wamepata dawa zinazotibu magonjwa mengine pia zinaweza kutibu ugonjwa huu.
Dawa zinazotibu maradhi ya moyo, mfadhaiko na kifafa zimepatikana kutibu kipandauso katika vipimo tofauti vya dawa hizo.
Ila hizo huja na madhara yake, na hufanya kazi kwa njia tofauti kwa kila mmoja.
Huenda mafanikio makubwa zaidi katika matibabu ya kipandauso yalikuja wakati wanasayansi walipofuatilia kwa karibu molekuli zinazopatikana katika mishipa ya damu iliyo karibu na ubongo.
Molekuli za akili
Mwanzoni mwa miaka ya 1990, wanasayansi walichukua sampuli za damu kwa kutumia sindano kutoka kwenye mishipa ya shingo (jugular veins) ya wagonjwa 32.
Damu hiyo, iliyokuwa ikirudi kuelekea moyoni baada ya kuzunguka kwenye ubongo, ilikuwa imejaa vipande vingi vya protini vilivyoitwa calcitonin gene-related peptides, au CGRPs.
CGRPs ni protini ndogo zinazofanya kazi kama vitufe vya kuongeza au kupunguza shughuli na usikivu wa seli za neva.
Wakati wa shambulio la kipandauso, protini hizi huonekana kwa viwango vya juu sana, zikitanda kwenye seli za neva na kuongeza usikivu wake, anasema Debbie Hay, profesa wa famasia na taaluma ya sumu katika Chuo Kikuu cha Otago, New Zealand.
Tafiti zinaonyesha kwamba viwango vya CGRP huwa juu zaidi katika damu ya watu wanaougua kipandauso, hata pale wasipokuwa wanapata shambulio. Wanasayansi pia wamefanikiwa kuweza kuchochea mashambulio ya kipandauso kwa kuwachoma wagonjwa sindano zenye CGRP za ziada.
Kuzuia kipandauso
Kuzuia CGRP kunaweza kusaidia kusitisha shambulio la kipandauso linaloendelea,kwa kurejesha hali ya kawaida, anasema Hay.
Ingawa hili halimaanishi moja kwa moja kwamba kemikali za peptides ndizo chanzo cha msingi cha kipandauso, zinawakilisha utaratibu halisi wa kibaolojia wa kupunguza ishara nyingi kupita kiasi zinazosababisha dalili za ugonjwa huo.
"Kimsingi, kila kitu huja kwa sehemu ya kuzima na kuwasha ipo wapi" anasema Amynah Pradhan, mkurugenzi wa taaluma ya madawa
katika Chuo Kikuu cha Washington, Marekani.
Kutokana na kugunduliwa kwa utaratibu huu, dawa nane zinazolenga CGRP tayari ziko sokoni, baadhi hutumia kingamwili zinazofyonza CGRP yote iliyo kwenye damu, na nyingine huzuia peptides kuamsha seli za neva.
"Hizi bila shaka zimeleta nafuu kubwa kwa wagonjwa wa kipandauso," anasema Pradhan. "Zimepanua wigo wa suluhisho zinazopatikana."
Utafiti mmoja wa mwaka 2025 ulibaini kwamba 70% ya watu waliotumia dawa za CGRP kwa kipindi cha mwaka mmoja waliona mashambulio yao ya kipandauso yakipungua kwa 75%, huku 23% wakikosa kupata kuathirika na ugonjwa huo.
Utafiti mwingine uliofanywa na timu hiyo hiyo uligundua kuwa idadi ya watu waliopata nafuu kutokana na matibabu ya CGRP iliongezeka kadri miaka ilivyozidi kusonga, baada ya mwaka wa kwanza, takribani 50% ya wagonjwa waliona mashambulio yao yakipungua, lakini baada ya miaka mitatu, 70% ya wagonjwa walinakili kuwa kuathirika kumepungua.
Ingawa baadhi ya wagonjwa hunufaika sana na matibabu ya CGRP kiasi cha kuitwa "wanaopata nafuu haraka" (super-responders), wengine hawapati manufaa yoyote kabisa.
Ujio wa dawa mpya
Hata hivyo, ugunduzi wa CGRP umeweka msingi wa kuibuka kwa kundi jipya la dawa. Neuropeptides nyingine, kama Pacap (pituitary adenylate cyclase–activating polypeptide), zimegunduliwa kuwa na mchango mkubwa katika kutibu kipandauso.
Ingawa Pacap ni kundi tofauti la peptides zinazofungamana na aina tofauti ya vipokezi kwenye seli za neva , kuwachoma wagonjwa wa kipandauso Pacap mara nyingi huchochea shambulio, ilhali kingamwili dhidi ya Pacap huleta nafuu.
Matibabu mengine
Uvumbuzi mwingine wa hivi karibuni unatokana na kutambua kwamba bidhaa inayotumika zaidi kwa madhumuni ya urembo inaweza pia kuleta nafuu kwa wanaougua kipandauso.
Sindano za kuondoa mikunjo ya uso au Botox imetambulika kuleta nafuu kwa wagonjwa wa kipandauso
Wagonjwa ambao hudungwa sindano hizi, hupata nafuu na mashambulizi ya kipandauso hupungua
Ni mojawapo ya "tiba zenye ufanisi zaidi tunazoweza kuwapatia wagonjwa," anasema Kissoon. Yeye hudunga sindano 25 hadi 33 kwa kichwa na shingo na kichwa waathiriwa wa kipandauso mara mbili au tatu kwa mwaka











