'Katika kuvumbua kiatu hiki, nilitaka kutengeneza kitu cha kipekee'

Maelezo ya video, “Katika kuvumbua kiatu hiki, nilitaka kutengeneza kitu cha kipekee”
'Katika kuvumbua kiatu hiki, nilitaka kutengeneza kitu cha kipekee'

Teddy Omondi aliye na miaka 21 ameweza kubuni kiatu ambacho kina uwezo wa kucheza muziki, tochi ya kumulika gizani na pia Kiyoyozi cha kupozea miguu wakati wa joto.

Uvumbuzi huu wa kipekee @teddyjacobs_the_innovator anasema ulitokana na ndoto yake tangu utotoni wa kubuni kitu ambacho bado hakijavumbuliwa.

Matumaini yake ni kuwa ataweza kuwashawishi kampuni kubwa waweze kumfadhili ili aweze kupenya kwa solo la vijana ambao wanapenda burudani na kusikiza muziki mara kwa mara.

Video: @judith_wambare