Kwa nini wakulima wa korosho Tanzania wamegoma kuuza zao hilo?

Maelezo ya video, Moja ya sababu inayotajwa ni bei ya chini ya takriban dola 1
Kwa nini wakulima wa korosho Tanzania wamegoma kuuza zao hilo?
Korosho

Baadhi ya wakulima wa korosho mkoani Mtwara Kusini mwa Tanzania, wamegoma kuuza zao hilo katika msimu huu wa mavuno.

Moja ya sababu inayotajwa ni bei ndogo ya takriban dola 1 ambayo wakulima wanasema haikidhi gharama za kilimo. Korosho ni moja ya mazao yanayochangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa, huku serikali ya Tanzania ikinuia kupata tani laki 4 katika msimu wa mwaka 2022/23.