Viboko wa Pablo Escobar kuhamishwa kwa dola milioni 3.5

Maelezo ya video, Viboko mlanguzi wa dawa za kulevya Escobar kuhamishwa kwa dola milioni 3.5
Viboko wa Pablo Escobar kuhamishwa kwa dola milioni 3.5

Colombia imesema mpango wa kuwahamisha viboko 70 hadi kwenye hifadhi za ng'ambo utagharimu dola milioni 3.5.

Mlanguzi wa dawa za kulevya Pablo Escobar, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi mwaka 1993, aliingiza nchini kinyume cha sheria wanyama wa kigeni, wakiwemo viboko kadhaa, katika miaka ya 1980.

Kufuatia kifo chake baadhi ya viboko hao walitoroka na idadi yao kuongezeka, kuwa kundi kubwa zaidi la wanyamba hao nje ya Afrika.

Wamekuwa wakiteka mashambani karibu na shamba la Escobar la zamani.

Mamlaka zinatumai kuhamisha baadhi ya viboko katika miezi ijayo, huku 10 wakielekea Mexico na 60 wakienda India.

viboko