Tazama: Ndege ilivyoanguka huku mkuu wa Wagner akidaiwa kuwa miongoni mwa abiria
Tazama: Ndege ilivyoanguka huku mkuu wa Wagner akidaiwa kuwa miongoni mwa abiria
Picha zilizothibitishwa na BBC zinaonyesha wakati ndege ikianguka kutoka angani huko Kuzhenkino, Urusi.
Bosi wa Wagner Yevgeny Prigozhin alikuwa kwenye orodha ya abiria wa ndege iliyoanguka nchini Urusi na kuwaua watu wote 10 waliokuwa ndani.
Inaaminika kuwa alikuwa ndani ya ndege hiyo.
Ripoti zaidi sasa zinaonyesha kuwa miili nane imepatikana katika eneo la ajali, hiyo ni kwa mujibu wa shirika la habari la Urusi RIA Novosti, likinukuu huduma za dharura.



