'Mkate mmoja kwa familia ya watu 30': Bekari zinavyojitahidi kulisha watu wa Gaza

Maelezo ya video, Kati ya bekari 130 ya kuoka mikate zilizokuwa zinafanya kazi huko Gaza kabla ya vita, 11 zimeharibiwa na mashambulizi ya anga ya Israel.
'Mkate mmoja kwa familia ya watu 30': Bekari zinavyojitahidi kulisha watu wa Gaza

Maelfu ya watu wanakabiliwa na njaa huko Gaza huku chakula na maji yakipungua, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani limeonya.

Shirika hilo limeiambia BBC pekee kwamba kati ya bekari 130 ya kuoka mikate zilizokuwa zinafanya kazi huko Gaza kabla ya vita, 11 zimeharibiwa na mashambulizi ya anga ya Israel.

Zile zilizosalia haziwezi kufanya kazi kwa sababu ya uhaba wa mafuta na unga.

Mwandishi wa BBC Idhaa ya Kiarabu Adnan al-Bursh ametembelea baadhi ya viwanda vya kuoka mikate kusini mwa Gaza.

Ana ripoti ifuatayo ambayo inaonyesha kampuni za kuoka mikate zikijitahidi kuendana na mahitaji makubwa ya usambazaji muhimu wa mkate.