Fahamu punda wa mashindano anavyotunzwa

Maelezo ya video, Lamu: Fahamu punda wa mashindano anavyotunzwa
Fahamu punda wa mashindano anavyotunzwa
punda

“Kwa mwezi ili kutunza punda wangu, hunigharimu kati ya shilingi 6,000 (dola 60) na shilling 7,000 (dola 70). Ni ghali kweli lakini…Mahaba… Yamependa hapo” Omar Ahmed ni mmoja wa wamiliki wa punda ambao kazi yao ni moja tu, Kushiriki mashindano ya kukimbia katika kisiwa cha Lamu Nchini Kenya.

Ni mashindano ambayo huvutia maelfu ya wakazi pamoja na wageni wanaozuru kisiwa hicho ili kuhudhuria tamasha mbali mbali. Mwanahabari wetu @judith_wambare alitembelea makao maalum ambapo punda hawa wametengewa na kutuandalia habari hii.