Andile Dlamini: Muziki na mpira wa miguu ni 'mchanganyiko maalum'

Maelezo ya video, Tazama: Kipa bora wa Afrika azungumza soka na muziki
Andile Dlamini: Muziki na mpira wa miguu ni 'mchanganyiko maalum'

Andile Dlamini wa Afrika Kusini ndiye kipa bora wa kike barani Afrika na sasa anajiandaa kwa Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake.

Lakini mnamo 2021, kazi yake nusra isambaratike alipoambukizwa Covid-19.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 30 alizungumza na BBC kuhusu mapambano yake na virusi hivyo na jinsi anavyochanganya muziki na soka.