'Sikutaka kuzunguka mitaani na kikombe nikiomba omba'
'Sikutaka kuzunguka mitaani na kikombe nikiomba omba'
Ken Cheruiyot ni kijana wa miaka 19 nchini Kenya.
Tangu kuzaliwa ametumia magoti yake kutembea, kutokana na ulemavu wa viungo vyake ya miguu.
Licha ya hayo Ken anafahamika kama fundi hodari na uwezo wake hasa kurekebisha trela na lori ni wa kuenziwa.
Alizungumza na na mwandishi wa BBC Anne Ngugi alipotembelea karakarana yake Kaunti ya Bomet katika eneo la bonde la ufa nchini Kenya




