Shule inayotoa nafasi ya pili kwa wanafunzi waliopata mimba za utotoni Kenya

Maelezo ya video,
Shule inayotoa nafasi ya pili kwa wanafunzi waliopata mimba za utotoni Kenya

Shule ya Green land ni shule ya kipekee nchini Kenya , inatoa nafasi ya pili kwa baadhi ya wasichana walioko shuleni wanaopata mimba za mapema na kutelekezwa nyumbani au wasichana wanaoozwa katika ndoa za mapema au wasichana wanaojifungua baada ya kubakwa.

Mbali na kupata elimu hapa , pia wasichana hawa wanapata fursa ya kuishi na watoto wao wachanga katika mazingira ya shule .

BBC ilipata fursa ya kufika shuleni humo na kuzungumza na baadhi ya kinamama wadogo kuhusu kupata nafasi ya pili wamezungumza na Anne Ngugi.