Marubani wawinda makombora ya Urusi baada ya kufanya mashambulizi
Marubani wawinda makombora ya Urusi baada ya kufanya mashambulizi
Urusi imerusha mamia ya makombora na ndege zisizo na rubani huko Ukraine katika wiki chache zilizopita, na kuua makumi ya raia na kusababisha kukatika kwa umeme kote nchini.
BBC imezungumza na mmoja wa marubani wa kivita waliopewa jukumu la kujaribu kuzuia silaha hizo hatari kabla ya kushambulia miji ya Ukraine.
Anajulikana kwa jina la kubuni la “Juice”, kwasababu mamlaka imemtaka afiche utambulisho wake.



