'Rubani aliwasha taa wakati tunaokoa watu tukaambiwa ndege inaweza kulipuka'- shuhuda

'Rubani aliwasha taa wakati tunaokoa watu tukaambiwa ndege inaweza kulipuka'- shuhuda

Mmoja wa waokoaji anasema shughuli ya kuokoaji ilisitishwa baada ya waokoaji kuingiwa na hofu ndege ya shirika la Precision Air iliyoanguka kwenye Ziwa Victoria nchini Tanzania inaweza kulipuka.

William Ruta, mkazi wa Bukoba ni miongoni mwa mashuhuda waliohusika katika zoezi la uokoaji.