Kwa nini Israel inakumbwa na machafuko?
Kwa nini Israel inakumbwa na machafuko?

Sehemu ya kwanza ya 'mageuzi' ya kisheria imepitishwa katika bunge la Israel licha ya maandamano ndani na nje ya bunge hilo.
Israel imekumbwa na maandamano tangu mwanzoni mwa mwaka huu kutokana na hatua ambazo wakosoaji wanasema zitadhoofisha uwezo wa mahakama katika kuisimamia serikali ya mrengo wa kulia zaidi katika historia ya Israel.
Lakini Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu anasema mageuzi hayo ni muhimu kwa taifa.



