Wanawake wa Afghanistan wanaopinga utawala wa Taliban kupitia muziki
Wanawake wa Afghanistan wanaopinga utawala wa Taliban kupitia muziki

Waimbaji wa Afghanistan nje ya nchi hiyo wamekuwa wakitumia muziki kuonyesha uungaji mkono wao kwa watu wanaoishi chini ya Taliban. Video nyingi, ambazo kwa kawaida huchezwa na wanawake, husambazwa ndani ya nchi kwenye mitandao ya kijamii. Taliban walichukua tena udhibiti mnamo Agosti 2021 na wamekuwa wakiweka vizuizi vikali, haswa kwa wanawake.



