Mwalimu Pangoma: Nilitamani kuwa injinia lakini sikuweza kuendelea na masomo

Maelezo ya video, Mwalimu Pangoma: Nilitamani kuwa injinia lakini sikuweza kuendelea na masomo
Mwalimu Pangoma: Nilitamani kuwa injinia lakini sikuweza kuendelea na masomo

Mwalimu Yusuph Pangoma alijiriwa kama mwalimu mwaka 2018 baada ya kukaa nyumbani kwa miaka mitatu tangu alipohitimu chuo mwaka 2015 na kwa kipindi chote hicho alikua akijitolea kufundisha watoto wa ndugu na jirani zake Jijini Dar es salaam.

Alipowasili shule ya msingi Ikorongo wilaya ya Serengeti mkoani Mara hakufahamu kwamba angeishia kuwa mwalimu wa madarasa ya awali kwani alichosomea yeye hasa ni elimu ya msingi, lakini uhaba wa walimu ulimfanya mwalimu mkuu wa shule hiyo Joseph Jackson kumpangia darasa hilo kutokana na umri wake na mwonekano wake.

Mwandishi wa BBC Eagan Salla na taarifa zaidi...